Friday, 29 December 2017

POLISI YAMSAKA MDHALILISHAJI

Huko Mbagala Majimatitu jana 29 Dec 2017 imelipotiwa kuwa hali ilichafuka mitaani kwa yaliyojitokeza habari zinasema kuwa mwanamama mmoja (jina tunalihifadhi) ambaye ni mke wa bwana mmoja ambaye ni mfanya biashara alijiwa na bwana mmoja ambaye ni mtumishi wake akiwa nyumbani kwake na kumshambulia vikari lakini walipoingilia kati majirani wema majibu yakawa "huyu amechelewa sana kurudi "  kana kwamba amepewa mamlaka ya kumdhibiti na mume wake lakini la kustaajabisha mume alikuwepo ndani wakati yote hayo yanajiri siku mbele ndipo yalipo jiri haya mazito zaidi ya kwamba asubuhi 29 dec watu walipoamka walikuta picha zimebandikwa kila kona za mitaa zikiwa na ujumbe mbaya unaomhusu mwanamama huyo ukimtuhumu Kufanya biashara haramu ya kuuza mwili wake taarifa zikamfikia mwenyewe kabla hakuja pambazuka vizuri alipopewa habari zilizopo kuhusu kuchafuliwa huko alisema "Ninafahamu ni nani aliyefanya hivyo" akatoka na akaanza kubandua pamoja naywasamalia wema picha zake na matangazo yanayo muhusu baadae alifika kituo cha Kati cha polisi na kuripoti ilipofika alasiri msako wa polisi kumtafuta mtuhumiwa ulianza na kwa habari zilizopo alicharopoka bado haja kamatwa na mpaka sasa na pamoja na yote hayo kuna tetesi za kuwa hayo yote yamesababishwa  na wivu wa mapenzi japo kuwa sio taarifa rasmi ila tukio la kuchafuana ni baada ya mfanyakazi huyo kuoa mke siku moja mbele.

No comments:

Post a Comment

MADHARA NA FAIDA YA KITUNGUU MAJI

Na Imaam Jafari Mtavassy As, alaykum ndugu wasomajia na wapenzi wa blogg yetu hii pendwa leo nimechagua katika elimu ya tiba niongelee jamb...